Mwenyekiti wa UVIWAMA Nditi, ndugu Suleiman Piku amemuomba Mgeni rasmi kutoa tamko rasmi kuhusu mustakabali wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha nditi walayani Nachingwea, hayo yamesemwa leo June 14, 2025 katika kilele chaMaonesho ya Madini Mkoa wa Lindi yanayafanyika Mjini Ruangwa.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba wanashindwa kuongeza miundombinu katika eneo lao la uchimbaji kutokana na kukosekana kwa leseni itakayowarasimisha na kua wachimbaji rasmi katika eneo hilo wanalofanyia shughuli zao
Ameongeza kua katika maonesho haya ya madini wameweza kua wadhamini wakuu wa maonesho jambo ambalo wanalifurahia kwani linaongeza fursa kwa wachimbaji hao.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.