ZAO la asili la upupu ambalo limekuwa chakula pendwa kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambalo mara nyingi huliwa kama futari na wananchi wa mikoa hiyo.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa zao hilo wameamua kuanza kuhifadhi mbegu zake kwa kuwa limeanza kupotea hivyo hawapo tayari kupoteza chakula chao cha asili na pendwa.
Wananchi walisema chakula cha upupu ukikosea kukianda hugeuka kuwa sumu kwa sababu za kukosea maandalizi yanayotakiwa wakati wa kupika chakula hicho.
Kwa upande wake afisa miradi mwandamizi kutoka SWISSAID Veronica Masawe alisema kuwa upupu chakula ambacho kina virutubisho vingi mwilini lakini usipopika kwa utaratibu hugeuka kuwa sumu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.