Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. @hashim_komba akimsikiliza Mzee maarufu kutoka kata ya Namapwia Mohamed Nambitile baada ya kikao cha viongozi wa dini, Siasa na Wadau mbalimbali kilichobeba ajenda kuu ya Sensa ya watu na Makazi ya Agosti 23, 2022..
Mzee Mohamedi pamoja na hoja ya msingi ya Sensa alihoji kuhusu hatua zilizofikiwa na Serikali kuhusu Tembo .
Mhe. Komba alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali na zinazoendelea kuchukuliwa ikiwemo kuanza kuwaondoa Mifugo hasa Ng'ombe waliovamia katika hifadhi ya wanyama pori.
Licha ya hatua, hiyo Mhe. Komba ameeleza kutokana na athari za wanyama hao Serikali imeshaandaa utaratibu wa kutoa chakula (Mahindi) yatakayouzwa kwa bei nafuu ili kila mmoja aweze kumudu kuyapata.
#jiandaekuhesabiwaagosti23,2022
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.