“Tasaf imeniwezesha kujikwamua kiuchumi” Bi Hadija Sefu
Bi Hadija Sefu mkazi wa kijiji cha Namikango A ameeleza kunufaika na mradi wa Tasaf kwa kujenga nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ambayo pia imeunganishwa na nishati ya umeme wa jua.
Akielezea namna alivyoweza kujenga nyumba hiyo Bi Hadija alisema alikuwa anajiwekea akiba kwa kile alichokuwa akipata,hatimaye alijikuta amepata fedha za kununulia bati,boriti na kuweka nguvu katika ufyatuaji wa tofali.
“Nilitengeneza kibubu nikipata elfu 32,000 natumia elfu 2,000 na kuweka elfu 30,000 japo nilianza kiasi cha shilingi elfu 28,000. Kwa kujiwekea akiba nimeweza kujenga nyumba hii ya vyumba vitatu ambamo ninaishi kwa sasa”.
Akielezea ujenzi wa nyumba yake imechukua takribani ametumia takribani mwaka mmoja kukamilisha shughuli za ujenzi hata hivyo amedai haikuwa kazi rahisi kwake kukamilisha ujenzi huo.
Aidha amewataka wanufaika wenzie kuzitumia fedha hizo vizuri kwani zinaweza kuwakwamua kiuchumi kwa kujenga makazi bora, kuanzisha biashara ndogondogo na kupunguza utegemezi na hata mradi utakapomaliza muda wake watakuwa na cha kujivunia.
“Fedha hizi sio ndogo mtu anaweza kuonesha kitu cha maana bali watu wengi wamekuwa wakizitumia fedha hizi kunywea pombe kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mradi huu wa kunusu kaya masikini”.
Aliongeza kwa kuwashauri wanufaika wenzie kuweka akiba na pia kujishughulisha na shughuli nyingine za uzalishaji mali na kutotegemea fedha za ruzuku pekee kama chanzo cha mapato.
Mradi wa kunusuru kaya maskini umeanza Februari 2014 kwa sasa unanufaisha kaya 5424 ambapo unagharimu kiasi cha shilingi 151,040,000 kwa mwezi
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.