Soko kuu Nachingwea kukarabatiwa
Baraza la madiwani limeazimia kukarabati soko kuu la wilaya ambalo limekuwa likilalamikiwa na wafanyabiashara na wateja wanaotumia soko hilo kutokana na uchakavu.
Azimio hilo lifikiwa katika mkutano wa kawaida wa Baraza la madiwani liliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba katika ukumbi wa Halmashauri mwishoni mwa wiki.
Akitoa ufafanuzi juu ya ukarabati wa soko hilo Mkuu wa Idara ya ujenzi na zimamoto Sospiter Chacha amesema kazi hiyo itafanyika kwa muda wa wiki kumina mbili hadi kumalizika (12) kuanzia tarehe 12.11.2018, maeneo yanayokarabatiwa ni sehemu ya kuuzia samaki, eneo la mama lishe na wauza mboga
Kufuatia ukarabati wa soko hilo wafanyabiashara wafanyabiashara watahamishiwa katika masoko ya Voda na Mbagala (Tunduru ya Leo).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo Arbogast Kiwale akielezea kuhusu kukamilika kwa masoko watakayohamia wafanyabiashara hao amesema masoko hayo yanakarabatiwa na yataisha kwa wakati na wafanyabiashara hao watahamia kwa wakati.
“Mheshimiwa Mwenyekiti mpaka kufikia tarehe 11.11.2018 ukarabati wa masoko ambayo wafanyabiashara watahamia yatakuwa yamekarabatiwa hivyo kuwawezesha wafanyabiashara hao kuhamia kwa wakati” Arbogast Kiwale
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.