Spika wa Bunge Mstaafu Mheshimiwa Anna Makinda ambae ni Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Tanzania bara amesema Sensa ya 202 ilikua ni Sensa ya ya kihistoria na ya kipekee ukilinganisha na sensa zilizopita, sensa hii ilikua ni ya kidigitali, hayo ameyasema alipokua katika Mafunzo ya Ufunguzi wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
Screenshot_20240731_090709_Instagram.jpg
Aidha, Bi. Makinda amesema mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya sensa hiyo yametolewa pia katika makundi tofauti na Sensa hiyo imeonesha kuwa na vijana wengi kuliko wazee.
Kutokana na Sensa hiyo katika mkoa wa Lindi wilaya ya Kilwa inaongoza Kwa kuwa na idadi ya watu 315,117 Nachingwea 233,665, Ruangwa 199,283 Lindi 185,618 Mtama 177,561 na Liwale ndiyo Halmashauri yenye idadi ndogo ikiwa na jumala ya wakazi 146,208.
Huku mkoa wa Lindi una jumla ya 8.6% ya tegemezi huku Halmashauri ya Mtama ikiongoza kwa 10.7% na Halmashauri ya Kilwa ndiyo yenye asilimia ndogo Katika mkoa wa Lindi kwa 6.4%, hivyo Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa minne nchini Tanzania yenye asilimia ndogo ya tegemezi kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
#tupovizuri
@nbs.tanzania
@owm_tz
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.