Wakulima wa Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI leo, 27 Julai 2025 wamefanya mnada wa saba na wa mwisho wa zao la ufuta kwa msimu huu uliofanyika makao makuu ya chama hicho, Nachingwea.

Katika mnada huo, bei ya juu imefikia Sh 2,500 kwa kilo na ya chini Sh 2,410, ambapo jumla ya kilo 922,703 kutoka maghala ya wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale zimeuzwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Mohamed Hassan Moyo, Balozi Mbarouk, Katibu Tawala wa Wilaya, amepongeza chama hicho kwa kusimamia vyema minada yote saba bila changamoto kubwa na kuwataka wakulima waendelee kuwa waaminifu ili kuvutia wanunuzi.

Wakulima nao wamefurahishwa na bei zilizopatikana na usimamizi wa chama hicho, huku wakihimiza juhudi za kutafuta masoko bora zaidi kwa msimu wa mbaazi unaofuata.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.