RUNALI KUFANYA MNADA WA MBAAZI MARA MBILI KWA WIKI, JUMATANO NA JUMAPILI
Ndg Emanuel Wilbard afisa Masoko wa Chama Kikuu cha ushirika Runali amesema hayo Agosti 21, 2024 alipozungumza na wahandishi wa habari kwenye mnada wa pili wa Mbaazi uliofanyika makao mkuu ya Runali Nachingwea.
Amezungumzia sababu ya kufanya minada miwili ndani ya wiki moja tofauti na utaratibu uliozoeleka wa mnanda mmoja kwa wiki. Amesisizitiza kwa kusema Mbaazi nizao ambalo alichelewi kuingiliwa na wadudu,wamefanya hivyo ili waweze kuuza mbaazi zikiwa kwenye ubora.Amewatoa shaka wakulima waliouza mnada wa jumapili watapata kutokana na bei zilizojitokeza jumapili na wale waliuza jumatano pia.
Wakulima wamefurahishwa na bei za mnada wa jumatano wa Sh 1880 bei ya juu na Sh 1840 bei ya chini matamanio yao bei zisishuke ili waweze kupata fedha zitakazo wawezesha kuboresha kilimo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.