Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka ameonesha kufurahishwa na kupongeza jitihada za Uongozi wa Halmashauri ya Nachingwea kwa kitendo cha kwenda Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Tanganyika kwa ajili ya kujifunza biashara ya Carbon (Carbon Credit).
Mhe Mtaka amewasisitiza timu hiyo kuhakikisha wanatekeleza kile walichojifunza na kukusudia ili kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na kuwaletea maendeleo wananchi wa Nachingwea na Tanzania kwa ujumla.
Aidha, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea bw. Lington Nzunda amemshukuru Mhe Mtaka kwa kutoa pongezi na kuwasisitiza kutekeleza mradi huo, Nzunda amesema "Halmashauri imezamilia kufanya biashara ya Hewa Ukaa na hasa lengo ikiwa ni kuongeza pato la halmashauri ili kuweza kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya ya Nachingwea".
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.