(RAMATA) Rafiki wa Mazingira Tanzania rasmi wametambulisha mradi wa utunzaji Mazingira Mkoa wa Lindi wilaya ya Nachingwea Kwa kupanda Miti katika Chanzo Cha Maji cha Mkumba Kata ya Mpiruka, zoezi hilo limefanyika siku ya Mazingira Duniani, June 5, 2024.
Lengo la Mradi huu ni Kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kukabiliana na uharibifu wa Mazingira na Uoto wa Asili, hivyo kwa pamoja wanatekeleza wajibu wa Kulinda misitu, mito na kufanya usafi wa Mazingira.
RAMATA wataanzisha Benki za Miche katika kata zote ili kuhamasisha upandaji miti ili kuhakikisha Kasi ya upandaji miti inaongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi Kasi ya ukataji miti inayopo katika maeneo tofauti tofauti.
Aidha, RAMATA wataanziasha GREEN ENERGY asilia ili kuwahamasisha wananchi kutoka katika matumizi ya mkaa na kuni na kutumia nishati mbadala, RAMATA ni mkombozi wa Mazingira, pia
wanatunza Mazingira Kwa kufanya usafi na
wanafanya makongamano ya Kutoa Elimu ya Umuhimu wa Kutunza Mazingira..
Kauli mbiu ikiwa ni;
"Tunza mazingira Kwa maisha bora. Kila mwanadamu ni Mlinzi wa Mazingira."
#tukovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.