wafanyakazi kutoka ofisi na taasisi za umma na binafsi wakiwemo wa wafanyakazi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika maandamano ya Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 ambayo Kimkoa yanafanyika Liwale katika viwanja vya ujenzi
Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe. Goodluck Mlinga akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack,
Viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa Wilaya wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala, viongozi wa Taasisi na dini wameshiriki maadhimisho hayo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Mei Mosi 2025 inasema " Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya wafanyakazi , Sote Tushiriki "
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.