Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zimepata watumishi wapya kutoka Serikali kuu kwa mchanganuo ufuatoa Idara ya Afya watumishi 33, Idara ya Elimu Msingi watumishi 27, na Elimu Sekondari Watumishi 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa na menejimenti yote inawakaribisha Sana Nachingwea .
Aidha, Mkurugenzi na menejimenti yote inamshukuru Mhe. Rais licha ya uboreshaji wa huduma za Afya, Elimu na miundombinu mingine, ameendelea kutulea watumishi kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na Uhakika wakati wote .
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.