Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Ndugu Yefred Mayenzi, ametoa elimu ya kina ya namna ya upatikanaji wa mapato yatokanayo na ushuru wa madini kwa wataalamu kutoka kijiji cha Nditi wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.
Halmashauri ya Geita imeeleza namna migodi inavyotoa fursa kwa vijana. Hayo yamesemwa na Afisa mipango wa halmashauri ya Manispaa ya Geita Ndaro N. Samson, kwamba licha ya mapato yanayopatikana na halmashauri lakini pia wanaajiri vibarua kutoka katika vijiji vinavyozunguka migodi hiyo.
Katika ziara iliyofanywa na Wataalam pamoja na Viongozi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Kijiji cha nditi wamepata nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji migodi ikiwa katika kata ya Nditi kuna migodi mbalimbali inayotoa madini kama Nickel, Iron, copper na mengine.
Aidha Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Ndugu Lington Mzunda amemshukuru Mkurugenzi Mayenzi na Menejimenti nzima ya halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa mapokezi mazur na elimu waliotoa kuhusu uendeshaji wa migodi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.