Mratibu wa Mradi wa BOOST wilayani Nachingwea Ndg. James Katumbi amewataka viongozi wa serikali zaa vijiji vya Kiegei A kilichopo kata ya Kiegei na kijiji cha Chimbendenga kilichopo kata ya Mbondo kuhakikisha wanakuwa wawazi katika hatua zote za mradi kwa kuwapa taarifa wananchi. Hayo ameyasema April 2, 2023 alipotembelea vijiji hivyo akiwa na kamati ya Mradi wa BOOST wilayani humo.
Aidha, Ndg. Katumbi amesema kwa kuwashirikisha wananchi katika mradi huo, kutapelekea kudumisha ushirikiano kati ya serikali na wananchi katika kutekeleza mradi huo na kufanya mradi kukamilika kwa wakati na kuondoa migogoro.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.