Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mheshimowa Mohamed Hassan Moyo amepongeza Kata ya Kilimarondo na kijiji cha Kilimarondo kwa kuanzisha mnada wa ng'ombe utakaotumika kuuzia wanyama hao, hayo ameyasema Septemba 4, 2024 alipofanya ziara katika kata hiyo.
Mhe Moyo amewapa pongezi sambamba na kuwasihi wananchi kutumia hiyo kama fursa katika kujiingizia kipato kwa kufanya shughuli mbalimbali katika eneo hilo kama mama lishe na kuchoma nyama kwani eneo litakutanisha watu kutoka maeneo ya Wilaya za Tunduru, Masasi na Nachingwea.
Pia katika biashara hiyo, kata, kijiji na Halmashauri vitapata mapato kutokana na mnada huo, hivyo eneo ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa na kufanyiwa uwekezaji nzuri na kulifanya eneo kuweza kufanya kazi kwa kudumu.
Aidha, sambamba na hayo wamewataka wkazi na uongozi wa Kata hiyo kuendeleo kuandaa eneo hilo lakini kwa kuzingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi na utunzaji wa misitu kwani hata hivyo kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji 16 vilivyopo katika mpango wa biashara ya hewa ukaa na misitu ndio msingi wa biashara hiyo yenye faida kubwa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.