Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, ameongoza mbio za ridhaa za kilometa 5 zilizofanyika leo Juni 12, 2025, katika wilaya ya Ruangwa, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea maonesho ya Lindi Mining Expo 2025.
Mbio hizo zimeshirikisha wananchi kutoka Ruangwa na maeneo mengine ya Mkoa wa Lindi, zikiwa na lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii katika maendeleo kupitia sekta ya madini.
Tukio hilo limeashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya maonesho, na limewajumuisha wadau kutoka sekta binafsi, taasisi za serikali na wananchi kwa ujumla, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na kuongeza uelewa kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya madini.
Maonesho ya Lindi Mining Expo 2025 yanaendelea hadi Juni 14, yakilenga kuonyesha rasilimali za madini, kuhamasisha uwekezaji na kukuza ushirikiano wa wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.