Mkuu wa Divisheni Elimu Sekondari Mwalimu Andrew Mhulo wa Halmashauri ya Nachingwea amewataka walimu, bodi za shule na uongozi wa Tarafa na kata wilayani humo kushirikiana katika kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na madarasa mengine wanaripoti shuleni kwa wakati. Hayo amesyasema January 9, 2024 alipokua katika zoezi la ufuatiliaji wa uripoti wa wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Aidha, Mwalimu Mhulo ameipongeza Sekondari ya Chiola pamoja na uongozi wa kata hiyo kwa kufanya idadi kubwa ya watoto kuripoti shuleni ikiwa ni siku ya pili tokea Shule zilipofunguliwa. Pia, amewaagiza walimu viongozi wa Sekondari zote Wilayani Nachingwea kuhakikisha wanaendana na mpango wa kitaifa wa kufaulisha kwa zaidi 50% ya wanafunzi waliopo katika darasa husika kwa ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.