Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telack akizungumza katika maadhimisho ya kilele Cha siku ya wanawake Duniani ameeleza kuwa Mkoa wa Lindi utaendelea kuwawezesha wanawake katika nyanja zote ili waweze kufikia malengo . " Tayari tumetoa fedha sisi Kama Mkoa Milioni 848. 7 kwa ajili ya kuvipa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu 241 , ninawaomba Sana fedha hizi tuzitunze na kuzifanyia biashara vizuri ili ziweze kutunufaisha " Mhe. Telack
Aidha,Mhe Telack ameeleza kuwa Mkoawa Lindi umetenga tena fedha zingine kiasi Cha Milioni 427.4 ambazo zitatolewa kwa vikundi 86. Mhe. Telack amewasisitiza akina Mama kuchangamkia fedha hizo kwa kuunda vikundi na kuziomba fedha hizo kwa ajili ya kujiendeleza .Sambamba na hilo, amewasisitiza akina mama kuwa na uadilifu, uaminifu na juhudi katika kazi ambayo ndiyo msingi wa mabadiliko chanya ya Jamii .
Sambamba na hilo Mhe. Telack amewataka wazazi /walezi wakike kufanya ufuatiliaji kwa watoto kila siku na kila mahali ambapo watoto wanapokuwa.
Katika maadhimisho hayo , wanawake kutoka makundi mbalimbali wameweza kuonesha uwezo na shughuli zao mbalimbali za kila siku katika kujitafutia kipato ama kujiinua kiuchumi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.