Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack amewataka wazazi wilayani Nachingwea kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha wanawapeleka Watoto wao shule ili kuwapatia haki zao za kimsingi. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo alipokua katika mkutano na watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kilichofanyika February 15, 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Chuo cha Ualimu (TTC) wilayani humo.
Bi. Telack amewakumbusha wataalamu na wazazi katika wilaya hiyo kuwa serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya vitu vingi katika sekta ya elimu ili kurahisisha upatikanaji wa elimu kama vile kufuta ad ana kutengeneza miundombinu ya kisasa na imara. Hata hivyo serikali haiwezi kufanya kila kitu, hivyo wazazi ni lazima watekeleze majukumu yao ya kuwanunulia vifaa vya kusomea na kuwapeleka shule.
Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo amewakumbusha wazazi kuwa serikali haitoweza kuwavumilia wazazi ambao kwa namna moja au nyingine wanawashinikiza Watoto wao kujifelisha katika mitihani yao ili kukwepa majukumu yao.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.