Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Hashim A Komba amezindua mpango harakishi na shirikishi wa chanjo ya UVICO-19 leo Septemba 30, 2021 , uzinduzi huo umeshirikisha viongozi wa dini, watendaji wa kata, waheshimiwa madiwani, viongozi wa boda boda na wadau mbalimbali .
Katika uzinduzi huo, Mhe. Komba amewataka viongozi wa kata kufanya vikao kabla ya vikao ya kwenda kutoa elimu ngazi ya vijiji na vitongoji vitakavyoshirikisha wananchi. lengo, wananchi wapate eilu ya kutosha juu ya umuhimu wa chanjo ya UVICO-19 na madhara ya kutokuchanja .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.