Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Selemami Jafo amefanya ziara ya kikazi ya kukagua kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali wilayani Nachingwea leo September 19 2024.
Waziri Jafo ameagiza kituo cha Afya Lionja kuanza kutoa huduma ndani ya miezi miwili lengo kuwaondolea wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya ambapo kituo hicho kitakuwa na jengo la OPD jengo la nje pamoja na kichomea taka hivyo kitahudumia kata za jirani ambazo ni Namikango, Ngunichile na Nditi , zaidi ya shillingi milllion 400 zimetolewa na Halmashauri hiyo kupitia mradi wa ndani.
Aidha alitembelea katika kituo kipya cha Afya kinachoendelea kujengwa chenye jina KASSIMU MAJALIWA kinachojengwa katika kata ya Chiola chenye thamani ya shillingi million 193,4021480 hivyo mpaka sasa million 50,70700 zimekwishatumika kwenye ujenzi huo bado ujenzi unaendelea na kuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kufuatilia hati na kupatikana ndani ya mwezi mmoja lengo kupata fedha kwaajili ya kumaliza ujenzi huo hivyo zaidi ya miaka 47 walikuwa na zahanati pekee hali iliyopelekea wananchi kufuata huduma za Afya Katika hospital ya mnero na kutembea km 35 hadi kuifikia hvyo kituo hicho kitahudumia wakazi 6599 na kupunguza vifo vya mama na mtoto
Katika hatua nyingine alifika katika hospital ya wilaya na kuweka mawe ya msingi katika jengo la ICU ambalo lina thamani ya zaidi ya millioni 250 pamoja na jengo la OPD lenye thamani ya millioni 423,925,630, hivyo ujenzi wa jengo la kufulia, maabara, pamoja na kichomea taka vina thamani ya millioni 900 sambamba na uwepo wa wodi yenye thamani ya millioni 80 ambazo zinatokana na mapato ya ndani ya halmashauri.
Sambamba na hayo akitoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi nzuri wa ujenzi wa miradi hiyo na kuwapa salamu za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.