Tarehe 11 Juni 2025, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainabu Telack, amesema kuwa maonesho ya pili ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Madini, Wilaya ya Ruangwa kuanzia Juni 11 hadi 14, yameendelea kuonesha mafanikio makubwa katika kuchochea maendeleo ya sekta ya madini na uchumi wa mkoa kwa ujumla.
Mkoa wa Lindi umebarikiwa ardhi yenye utajiri wa madini mbalimbali, jambo linaloendelea kuwanufaisha wananchi kiuchumi na kijamii.
Amesema kuwa maonesho ya awali yalihusisha zaidi ya watu 6,000 na wageni kutoka mataifa 14, huku mwaka huu matarajio yakiwa ni kupokea washiriki wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi, wanaokuja kuona fursa zilizopo na kuwekeza.
Mhe. Telack amebainisha kuwa lengo la maonesho haya ni kuwaunganisha wachimbaji na wawekezaji, kuongeza ujuzi, kupanua mitandao ya kibiashara, na kuendeleza uchumi wa wananchi na taifa.
Amewapongeza wachimbaji kwa mchango wao mkubwa katika sekta ya madini na kuwataka waendelee kushirikiana na serikali katika kukuza na kuimarisha sekta hii kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kaulimbiu ya 2025: “Madini ni Uchumi, Shiriki Kuijenga Tanzania Yetu.”
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.