Makarani watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mheshimiwa Rukia Muwango amewaonya makarani wa vyama vya Msingi kuacha tabia ya kuwahujumu wakulima wa korosho katika maeneo wanayofanyia kazi.
Ameyasema hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi iliyokutana jana kujadili utekelezaji wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba 2017.
“Siko tayari tayari kuona mtu anadidimiza juhudi za mkulima hasa mkulima wa korosho ,baadhi ya makarani wanarubuniwa na baadhi ya wajumbe wa bodi kuhuwahujumu wakulima” Alisema Mheshimiwa Muwango
Aliongeza kuwa wapo baadhi ya makarani wanaandika stakabadhi kwa majina ya ndugu zao, ili kuineemesha wao kitu ambacho hakikubaliki kwa kuwa kina lengo la kumdidimiza mkulima.
Mkuu wa wilaya amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya wajumbe kulalamika kuwa baadhi ya wakulima kutoka maeneo yao kutolipwa fedha za mauzo ya korosho kwa msimu wa huu wa mwaka 2017/2018.
Akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya malamiko yaliyotolewa na wajumbe hao, Afisa Ushirika wilaya ndugu Lameck Chotta amedai wakulima wengi wamelipwa fedha zao, kwa wale wachache ambao hawajalipwa jitihada zinaendelea kuhakikisha kuwa wakulima wote wanalipwa. Baadhi ya viongozi wamefikishwa polisi kwa kwa taratibu za kisheria na wameanza kulipa fedha hizo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.