Makamo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ambae ni diwani viti maalumu kata ya Mpiruka (CCM) Mhe. Veronica D. Makotha July 26, 2023 amekabidhi zawadi kwa wanafunzi wawili Abdul Fakh na Teresia Wiliam ambao wamefanya vizuri katika mtihani wao wa kidato cha nne na kufanikiwa kujiunga na kidato cha sita ambao kila mmoja amepata kiasi cha fedha tsh 70,000/= na kufanya kwa wote wa wili kuwa Jumla ya Tsh 140,000/= kama motisha kwa wanafunzi waliobakia shleni hapo.
Aidha, Mhe Makotha amekabidhi taulo za kike (PADS) kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha tatu na nne katika shule ya sekondari ya Misufini pamoja na Mpira mmoja wa miguu katika Shule ya msingi Chiminula iliyopo kwenye kijiji cha Mpiruka A. kwenye kata ya Mpiruka. Mhe Makotha ameongeza kwa kusema ataendelea kuzitembelea shule hizo ili kuzifanya ziendelee kufanya vizuri kiwilaya,Mkoa na ata Taifa kwa ujumla.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.