• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko/mrejesho |
Nachingwea District Council
Nachingwea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii Vijana na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi na Zimamoto
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • TEHAMA
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Ugani
  • Madiwanii
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Mipango na Fedha
      • Ujenzi uchumi na mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari

MAFUNZO YA MAAFISA UGANI KILIMO YAFIKIA KILELE, YAKUSUDIWA KUBORESHA HUDUMA ZA UGANI KWA WAKULIMA

Imetumwa : January 17th, 2025



Mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa ugani kilimo walioajiriwa na Bodi ya Korosho Tanzania kupitia programu ya Jenga Kesho (Building a Better Tomorrow - BBT) yamehitimishwa leo, tarehe 17 Januari 2025. Mafunzo haya ya siku tano yalilenga kuboresha huduma za ugani kwa wakulima na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma bora za kilimo kupitia wahitimu wa fani ya kilimo.

Mgeni rasmi katika mafunzo hayo, Das Haji Balozi, akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Hassan Moyo, aliwasisitiza maafisa ugani kuwa na uadilifu katika kutekeleza majukumu yao na kutoa huduma bora kwa wakulima. Aliweka wazi malengo ya serikali ya Awamu ya Sita ya kuongeza uzalishaji wa korosho kwa kufikia tani 700,000 mwaka 2025/2026 na tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2029/2030. Aliipongeza Bodi ya Korosho kwa mafanikio yaliyopatikana, huku akisisitiza kuwa uzalishaji wa korosho ghafi umeongezeka kutoka tani 310,787 kwa msimu wa 2023/2024 hadi tani 410,000 kwa msimu wa 2024/2025.

Aidha, Mwenyekiti wa Runali Odas Mpunga, alitoa pongezi kwa maafisa ugani kwa juhudi zao za kuleta maendeleo katika kilimo cha korosho na kuhimiza ushirikiano zaidi kati ya wakulima na wataalamu wa ugani. Alisisitiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano wa karibu ili kufikia malengo ya serikali katika sekta ya kilimo na kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji.


Mafunzo haya yanalenga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo na kusaidia wakulima kuwa na ufahamu zaidi kuhusu mbinu bora za kilimo na uzalishaji wa mazao kwa wingi. Maafisa ugani walihimizwa kutumia pikipiki na Vishikwambi kama zana muhimu za kufikia wakulima wengi zaidi na kufanikisha malengo ya taifa katika kilimo cha korosho.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAOITWA KWENYE MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI March 26, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA WATENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 16 NA DERAVA DARAJA II NAFASI NNE May 25, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA AJIRA ZA UTENDAJI WA KIJIJI NA UDEREVA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA July 22, 2022
  • Tangazo la kazi za muda December 27, 2019
  • Angalia zote

Habari mpya

  • VIKUNDI 55 VYA WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% WAJENGEWA UWEZO

    July 03, 2025
  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% WATAKIWA KUWA NA NIDHAMU YA FEDHA, MILIONI 649 ZAKOPESHWA AWAMU YA PILI

    July 03, 2025
  • NACHINGWEA YAJIFUNZA MBINU BORA ZA USIMAMIZI WA MIGODI KUTOKA GEITA

    June 27, 2025
  • WATUMISHI LINDI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA USHIRIKI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KUJIFUNZA.

    June 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Wakulima wasisitizwa kulima mazao ya chakula
Video za mpya

Kurasa za Haraka

  • Opras Form
  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Eng. Chionda Alli Mfaume akizungumza waluu wa idara
  • MRADI WA MAJI NAMIKANGO WAZINDULIWA
  • Mpango wa Bajeti
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2021
  • UANZISHWAJI WA BLOCK FARMING WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
  • MRADI WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 1 WAANZA KUTEKELEZWA NAIPANGA
  • Sheria za Fedha za Mitaa
  • Sheria za Halmashauri

Tovuti mashuhuri

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • TUZO ZA ELIMU WILAYA YA NACHINGWEA
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.