wa Divisheni ya Elimu Msingi ndugu Stephen Urasa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari ndugu Hamphrey Kalisa wametoa pongezi na shukrani kwa Mbunge wa viti wa Maaalum Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Tekla Mohamed Ungele kwa kutoa misaada ya sare za shule, madaftari, viatu pamoja na peni kwa wanafunzi wenye uhitaji wa shule ya Msingi Ngunichile na Sekondari ya Ngunichile. Hayo yamefanyika February 28, 2024 walipokua katika ziara ya Mbunge huyo katika kata ya Ngunichile.
Katika ziara hiyo Mhe Ungele ametoa misaada ya sare za shule pea 20 kwa wanafunzi 8 wa kike na pea 12 wa kiume wa Sekondari ya Ngunichile, pia ametoa majola mawili ya vitambaa kwa ajili ya sketi na suruali na fedha taslimu Shilingi 100,000/= kwa ajili ya kushonea sare hizo. Vitu vingine ni viatu, madaftari na peni.Kwa upande wa shule ya Msingi Ngunichile Mhe. Ungele ametoa sare za shule kwa jumla ya wanafunzi 10.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.