Juni 11 2025 Maonesho ya pili ya madini yajulikanayo kama Lindi Mining Expo 2025 yamezinduliwa Wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, yakilenga kutangaza fursa za madini na kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Shaibu Hassan Kaduara, ambaye amesema sekta ya madini ina mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa, na serikali inaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya madini, kutoa ajira na kukuza uchumi.
Maonesho haya yanaongozwa na kaulimbiu:
"Madini na Uwekezaji: Fursa za Kiuchumi Lindi – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025."
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.