Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, amesema Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa maeneo machache nchini yaliyobarikiwa kuwa na madini ya kimkakati yenye thamani kubwa kiuchumi.
Ameyasema yao Juni 13, 2025, kwenye Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji (Lindi Mining Expo 2025), yanayoendelea Kilimahewa, wilayani Ruangwa.
Dkt. Kiruswa amepongeza maandalizi ya maonesho na ushiriki wa wadau mbalimbali, akisema yameweka msingi mzuri wa kukuza uwekezaji katika sekta ya madini.
“Lindi ni mkoa tajiri kwa madini ya kimkakati, nawapongeza kwa kazi nzuri,” amesema.
Maonesho haya yameelezwa kuwa jukwaa muhimu la kuibua fursa, kuimarisha ushirikiano na kuchochea maendeleo ya sekta hiyo mkoani Lindi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.