Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema lengo la mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ni kuongeza uwazi na uelewa wa matumizi wa matokeo ya Sensa 2022, hayo ameyasema alipokua Mgeni rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo iliyofanyika Julai 20, 2024 katika viwanja vya Kilimanihewa Wilayani Ruangwa.
Screenshot_20240731_090709_Instagram.jpg
Mhe. Majaliwa amewataka viongozi kuhakikisha Matokeo ya Sensa yanawafikia watendaji wa serikali na walengwa wote (wananchi) ili mipango ya maendeleo ionekane ikishamili kwa kutumia matokeo ya sensa hii, pia ameagiza ajenda ya usambazaji wa matokeo iwe ya kitaifa na kila kiongozi ajue idadi ya watu katika eneo lake.
Pia, Viongozi na watendaji wa serikali wametakiwa kukaa pamoja na kutafakari hatua walizofikia kulingana na matokeo ya sensa ili kuweza kutafuta mipango na mikakati sahihi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi na ndio kusudio hasa la sensa.
Mhe. Majaliwa amewaambia wananchi wa Mkoa wa Lindi kua Mkoa una fursa nyingi zinazowavutia wawekezaji hivyo ni jukumu la kila mwananchi na viongozi kutumia matokeo ya sensa kuangalia rasilimali zilizopo ili kuwavutia wawekezaji kwani matokeo ya sensa yanatumika kama fursa ya kupata ufahamu wa eneo gani la kuwekeza na wapi pa kufanya biashara gani kwani matokeo ya Sensa ya 2022 inaonesha kila kitu mpaka rasillimali zilizopo
Takwimu ni muhimu katika kupata uhalisia wa matumizi ya miundombinu na huduma mbalimbali katika jamii kwa kiwango sahihi na kujua mipango ya baadae kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla, pia amewasihi wananchi kutoharibu vibao vya anuani za makazi kwani ni muhimu kwa kupata maelekezo ya maeneo mbalimbali.
Aidha, Mhe Majaliwa amesema Mkoa wa Lindi kulingana na Matokeo ya Sensa ya 2022 una jumla ya watu 315,117 idadi hiyo imeongezeka ukilinganisha na matokeo ya sensa ya 2012, hivyo ni muhimu sasa Halmashauri, Wilaya na Mabaraza kwenda kwa kasi kulingana na ongezeko la watu.
#tupovizuri
@nbs.tanzania
@owm_tz
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.