Kiwanda kikubwa cha uchenjuaji madini ya Nickel, chenye miundombinu ya kisasa, kimejengwa Nditi, Nachingwea – hatua ya kihistoria inayotokana na juhudi za wachimbaji wadogo kupitia chama chao cha UVIWAMA. Mwenyekiti wao, Ndg. Mohamed I. Piku, amesema zaidi ya wachimbaji 700 wamezalisha na kusafirisha tani 68,400 za Nickel na Shaba, na kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 6.5 Ameyasema hayo , 11 Juni 2025, katika ufunguzi wa Maonesho ya Madini – Lindi Mining Expo 2025.
Kujengwa kwa kiwanda hiki ni utekelezaji wa maono ya serikali ya kuongeza thamani ya madini hapa nchini, sambamba na kukuza ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa Nachingwea na maeneo jirani.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.