Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Kiteto Septemba 2, 2024 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wamefanya ziara ya kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani katika Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kitendo Mheshimiwa Abdala B. Mohamed amesema lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kujifunza namna gani ya kuendesha mfumo huo wa uuzaji mazao maarufu kama stakabadhi ghalani kwa laengo la kuboresha masilahi ya wakulima wa Kiteto kwani kwa Halmashauri hiyo ndo kwanza wanaanza kutumia mfumo huo, Pia ametoa shukurani zake kwa wakazi wa Nachingwea kwa mapokezi mazuri na ukarimu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Hassan Losioki amewapongeza viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Nachingwea kwa ukarimu na mapokezi mazuri, pia amewasihi kufanya utekelezaji wa biashara ya hewa ukaa ambayo msingi wake ni utunzaji wa mazingira kwani wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa maeneo yanayonufaika na biashara hiyo.
Aidha, Afisa Kilimo (W) Ndugu Raphael Ajetu amewakaribisha na kuwaahidi kupata mafunzo mazuri kuhusu stakabadhi ghalani, pia amesema mfumo huo ulitambulishwa rasmi mwaka 2016 wilayani Nachingwea ambapo ulianza kutumika katika zao la korosho na ufuta na kwa sasa zao la mbaazi pia limeingia katika mfumo huo, lakini pia kuna vyama vya msingi 36 na maghala makuu manne.
Kwa upande wake Afisa Ushirika (W) Bi. Tunu Goagoa alipokua akitoa Elimu ya stakabadhi ghalani amesema kuwa katika biashara hiyo kuna uhakika wa soko, taarifa na bei kitu kinachopelekea wakulima kunufaika kwa misimu mitatu inayofuatana hata hivyo Nachingwea ipo katika taratibu za kuingiza zao la choroko katika mfumo huo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.