Priscus Silayo
Kilogram 438,687 za Korosho zauzwa
Wakulima wa korosho waliohudhuria kwenye mnada wa zao hilo wameridhia korosho zao Kilogramu 438, 687 kuuzwa kwa wafanya biashara mbalimbali.
Katika mnada uliofanyika jana katika viwanja vyao ofisi ya RUNALI jana kampuni 15 ziliweka zabuni zao, ambapo maombi 20 ya ununuzi wa korosho yalipokelewa
Baada ya kupitia barua hizo kampuni nne zilipitishwa kununua korosho kulingana na bei zao, bei ya juu ilikuwa Shilingi 2625 na bei ya chini 2567.
Awali akifungua mnada huo mwenyekiti wa RUNALI Ndugu Hassani Mpako aliwataka wakulima kufanya maamuzi ya busara katika kupitia kampuni zilizoonesha nia ya kununua korosho zao.
“Ninyi ndiyo wenye mali, tusikilize kwa makini bei zilizowekwa ili tufanye maamuzi mazuri kwa manufaa ya wakulima wetu” Alisema Mwenyekiti
Aidha, akiongea na wakulima waliohudhuria mnada huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amewataka wafanyabiashara walioshinda zabuni ya kununua korosho kulipa fedha mapema, wasipofanya hivyo watanyang’anywa mzigo huo.
“Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI baada ya kupokea malipo lipeni fedha moja kwa moja kwa wakulima ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza, makato ya AMCOS mnayafahamu” Aliongeza Mheshimiwa Zambi
Chama Kikuu cha Ushirika RUNALI kinaundwa na AMCOS za wilaya za Nachingwea, Liwale na Ruangwa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.