Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewataka wananchi kushiriki Uchaguzi wa serikali za Mitaa wa 2024, hayo ameyasema alipokua Mgeni rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo iliyofanyika Julai 2, 2024 katika viwanja vya Kilimanihewa Wilayani Ruangwa
Mheshimiwa Majaliwa amewasihi wananchi kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa kua Kila Mtanzania ana haki ya kuchaguliwa na kuchagua kiongozi anaemuhitaji katika uchaguzi na haki kimsingi na kisheria kwa kila mtanzania aliyetimiza vigezo.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kabla ya uchaguzi huo Julai 20, 2024 zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litafunguliwa hivyo wananchi wanapaswa kwenda kuhakiki uwepo wa taarifa zao ili kuhakikisha majina yao yapo ili kupata haki zao za msingi.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.