Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea Ndugu Omari Mwanga amewakumbusha viongozi wa idara ya Elimu Kusimamia misingi ya uwajibikaji na taratibu za Utumishi wa umma katika kufanikisha Malengo ya serikali ya kufuta sifuri na kuongeza ufaulu.
Katika kufanikisha malengo hayo katibu Tawala amewataka walimu waratibu Elimu kata na wakuu wa shule kuacha kujihusisha na ukusanyaji wa michango shuleni bila kibali maalum.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi, walezi na wadau wa kuwapeleka shuleni watoto wote ambao wamefikia umri wa kwenda shule na wale ambao tayari wameshaandikishwa au kuanza shule wasichelewe kuripot shule zitakapofunguliwa.
Katibu Tawala ameyasema hayo alipokutana na wakuu wa shule, waratibu Elimu kata, walimu wakuu na wadau wa Elimu kuelekea msimu mpya wa masomo 2022 ambapo shule zinatarajiwa kufunguliwa tarehe 17, Januari 2022.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.