Wananchi wameshauriwa kutumia karafuu inayopatikana wilaya ya Nachingwea ambayo inatibu matatizo ya kunuka mdomo na afya ya kinywa kwa ujumla.
Akizungumza katika maonyesho ya nane nane kanda ya kusini Neema Eliasi amesema kuwa watu wengi wanaokunywa pombe na wavuta sigara hunuka midomo yao mbele za watu ndio imekuwa sababu ya kutengeneza karafuu ya unga yenye mchanganyiko na virutubisho vya asili ambayo huondoa harufu mdomo.
Bi.Eliasi amesema kuwa karafuu hiyo pia hutibu tatizo la fizi kutoa damu wakati hata pata unapiga mswaki,hivyo ukitumia karafuu hiyo itakusaidia kutibu magonjwa hayo.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.