Leo Agost 26, 2024 Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) limeanza sherehe za mazimisho ya miaka 60 ambayo yatafanyika hadi Agosti 30, 2024 ambapo Jeshi hilo linatatoa huduma za matibabu bure kwa wananchi wa Nachingwea katika viwanja vya shule ya Msingi Majengo.
Katika viwanja hivyo Matibabu yanayotolewa ni Upimaji wa Sukari,Upimaji wa homa ya Ini, Upimaji wa Kaswende, Upimaji wa VVU, Upimaji wa shinikizo la damu(BP), Uchunguzi wa Kinywa na Meno, Uchunguzi wa Saratani ya tezi dume kwa njia ya damu, Uchunguzi wa Saratani ya matiti na Shingo ya kizazi pamoja na zoezi la uchangiaji damu.
Aidha, wanachi waliojitokeza katika eneo hilo wametoa shukurani zao kwa Jeshi la wananchi kwa kujali kutokana na sababu za kiuchumi wanachi wanashindwa kumudu gharama za matibabu hivyo inapotokea Jeshi linajitolea kwao ni jambo kubwa sana, pia wamefurahishwa na huduma zilizotolewa kwa unyenyekevu wao na lugha nzuri, pia Jeshi limewamewataka wakazi wa Nachingwea kuchangamkia fursa hiyo nakuacha tabia ya kusubiri siku ya mwisho kwenda kupata mababu kusababisho msongamano mkubwa.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.