"JIHADHARINI NA WAGENI WANAOINGIA KATIKA MAENEO YENU" ZAMBI
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe;Godfrey Zambi amewataka wananchi kuwa makini na watu wanaongia katika maeneo yao kwa kuwa kumekuwa na matukio ya uhalifu mikoa jirani na Mkoa wa Lindi.
Ametoa rai hiyo jana wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nammanga kata ya Ruponda alipokuwa akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kijiji hicho iliyojengwa kwa mapato yaliyotokana ushuru wa minara ya makampuni ya simu.
Amewataka wananchi kuwa makini na wageni hao kwani yawezekana wakawa ni wahalifu waliofanya uhalifu katika maeneo mengine na kuja huku kwa madai ya kutafuta mashamba au kutafuta wake.
“Tuwajue kwa uhakika wale wanaokuja ,tusiwajue kwa kanzu zao,kwa korani zao au biblia zao.Mkashawishika mkasema ni ndugu zenu,Dunia sasa imeharibika na watu wenye hila mbaya wanakuja kama watu wakarimu na rahimu sana kumbe ni watu wabaya kuliko samba au chui tuwe makini sana” Aliongeza Mkuu wa Mkoa.
Aidha Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi wa Kata ya Ruponda kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni ili watoto waweze kupata chakula shuleniili watoto wasome kwa bidii na kuongeza ufaulu wa shule za Msingi na Sekkondari.
Mkuu wa Mkoa alikuwa kwenye ziara ya kikakazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata za Namatula,Stesheni,Ruponda,Lionja,Nditi na Namapwia.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.