Eng. Khalifa Kitojo ambaye ni Kamanda wa TAKUKURU Nachingwea amewataka jamii za wafugaji kuepuka rushwa katika uchaguzi wa 2024 kwani rushwa ni kikwazo cha maendeleo, ameyasema hayo septemba 5, 2024
Pia, kiongozi huyo amewaomba wafugaji hao kutoa taarifa katika ofisi ya taasisi ya kuzuia rushwa pale wanapokutana na changamoto za rushwa katika jamii zao.
Aidha, amewasihi waweze kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kupata viongozi bora bila kuzingatia rushwa kwani viongozi bora ni chanzo cha maendeleo
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.