Halmashauri yapitisha Bajeti ya Shilingi bilioni 32
Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea imelenga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 32,197,359,990.78 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kutoka vyanzo mbalimbali.
Akisoma mpango na bajeti hiyo mbele ya Baraza la Madiwani lilofanyika jana kwenye ukumbi wa halmashauri, Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji Abdallah Nnunduma amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na mapato ya ndani ya halmashauri, ruzuku toka serikali kuu, miradi ya maendeleo, ruzuku kwa ajili ya mishahara, mapato kutoka kutoka shule mbalimbali na mapato kutoka huduma za afya.
Katika mpango huo Halmashauri inalenga kukamilisha miradi viporo, kuelekeza fedha kwenye miradi michache itakayotatua changamoto zilizopo kwa sasa, kukamilisha miradi ambayo inalenga kuongeza wigo wa mapato ya ndani ili kuiongezea halmashauri uwezo wa kujitegemea.
Aidha, Halmashauri inalenga kuimarisha usimamizi na ufauatiliaji wa miradi ya maendekleo na ukusanyaji wa mapato kupitia timu ya ufuatiliaji wa miradi miradi ya wilaya na kikosi cha ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Katika bajeti hiyo halmashauri imepanga kujenga kituo cha afya chenye thamani ya shilingi milioni 400 katika kata ya Mbondo na kukamilisha vituo vya afya vya Naipanga, Ngunichile na Namapwia.
Madiwani wamepongeza mpango huo kwa kuwa unalenga kukabiliana na changamoto mbalimbali kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.