Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Adinan Mpyagila Agosti 14, 2024 amefanya ziara ya kutembelea vituo viwili salama vya wanafunzi wa Shule za Msingi vilivyowekwa katika Shule ya sekondari ya Kutwa ya Nachingwea na Shule ya sekondari ya Farm 17.
Katika vituo hivyo kuna jumla ya wanafunzi 1016 kutoka katika shule tofautitofauti ambao wameonesha kutokua na alama nzuri za kufaulu na lengo ikiwa ni kuwasaidia ili wawese kufikia ufaulu wa alama A na waweze kujiunga ya Kidato cha kwanza.
Mhe. Mpyagila amewapongeza walimu kwa kujitoa na kufanya kazi ilyotukuka ili kuhakikisha wanafunzi hao wanatimiza malengo na kutekeleza lengo la Halmashauri la kuondoa alama E na F kwa Shule za Msingi zote na kuondoa Sifuri kwa Sekondari, pia amewapa zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani pamoja na kuwapa motisha ya shilingi 100,000 walimu katika kila kituo.
Kwa upande wake Afisa Elimu ya Watu wazima Bwana James Katumbi amesema mkakati huo umeanza kuonesha athari chanya kwani katika mitihani ya kwanza ya kujipima katika kituo cha Nachingwea Day walifaulu kwa 23% na mtihani wa pili 50%, pia katika kituo cha Farm 17 mtihani wa kwanza wamefaulu kwa 11% na mtihani wa pili 29% kwaio ni mategemeo mitihani ijayo wafaulu kwa zaido ya 80%.
Aidha, wazazi na wadau mbalimbali wameombwa kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Halmashauri ili kuenedele kuifanya elimu wilayani Nachingwea kua juu.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.