Halmashauri ya Nachingwea imetoa kiasi cha Shilingi million 19.3 kwa ajili ya utengenezaji wa viti na meza kwa lengo la kutatua changamoto ya viti na meza katika Shule za Sekondari za Halmashauri hiyo zilizoripoti upungufu wa viti na meza. Hayo yamesemwa leo January 16, 2024 na Mwalimu Johari Abdalah Mussa Mkuu wa Sekondari ya Nambambo wakati wa ziara fupi ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea ya ufuatiliaji wa uripoti wa wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Aidha, Mwalimu Johari ambae ni msimamizi wa mpango huo wa utengenezaji wa viti na meza amesema kiasi cha Shilingi million 19,350,000/= zimetolewa na Halmashauri kwa ajili ya utengenezaji wa viti 258 na meza 258 ambayo vitagawiwa katika shule zote ambazo zimeripoti upungufu mdogo wa viti na meza, pia Sekondari ya Nambambo ni miongoni mwa shule hizo.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.