Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea imeweka historia kwa kufunga mashine za virutubishi, ikiwa ni hatua ya kwanza katika kuboresha huduma za afya na lishe katika wilayani Nachingwea.
Mashine hizo zinatumia kilo moja ya virutubishi kwa tani mbili za unga, zitasaidia kuboresha usambazaji wa chakula na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za lishe, Mashine imefungwa katika kituo cha Al-qasmi Milling Machine iliyopo Kata ya Nangowe kijiji cha Matangini kitongoji cha Liwale B.
Akizungumza kuhusu mradi huu, Afisa Lishe Bi. Subira Omary Kambwili alieleza umuhimu wa mashine hizo katika kupunguza udumavu na kuhakikisha tunakua na afya bora asa kwa watoto, "hii ni hatua muhimu katika kuboresha afya na kupunguza ongezeko la watoto njiti" kwa Wilaya ya Nachingwea mashine imefungwa sehemu moja tu kwa kuanzia na baadae tutafunga na sehemu nyingine,".
Kwa upande wake Meneja Maendeleo na Biashara kutoka Sanku bwana Alpha Akimu, amesema kazi yao kubwa ni kuongeza virutubisho kwenye unga wa dona na sembe na wamekuja wilaya ya Nachingwea kufunga mashine moja kati ya mashine tatu zitakazofungwa Nachingwea katika mpango wa kutomeza udumavu na kuboresha lishe, Mashine hizo zimethibitishwa na shirika la viwango Tanzania TBS kuwa zitasaidia wananchi kuboresha afya zao na wafanya biashara kuongeza thamani ya unga wao..
Mfanya kazi katika kituo cha Al-qasi amesema "kwetu limekua ni jambo la furaha kuingia kwenye historia ya kuwa ofisi yetu imekua ya kwanza kufungwa mashine hiyo na tunawakaribisha wateja kuja kupata huduma na bei zetu ni zuri na tupo tayari kuwahudumia".
Akimywakilisha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Liwale B bwana Justan Mpinga amekiri kuwa jamii ilikuwa na matumaini makubwa na mradi huu na kwamba Mashine hiyo itasaidia kuboresha maisha afya katika jamii.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.