AFISA ELIMU MSINGI AONGOZA WATAALAM WA ELIMU WILAYA KUFANYA TATHIMINI YA IDARA YA MSINGI JANUARI HADI FEBRUARI 2023.
Mkuu wa Diveshini ya Elimu Msingi na awali Mwalimu Stephen Urassa ameongoza jopo la wataalam wa Elimu ngazi ya Wilaya kufanya tathimini ya miezi miwili kutoka Januari hadi fwbruari 2023 .
Tathimini hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Cha ualimu Nachingwea (TTC ) ukiwakutanisha maafisa Elimu kata, Walimu wakuu na wadhibiti ubora ngazi ya Wilaya.
Wataalamu hao wamepitia taarifa mbalimbali za ujifunzaji na ufundishaji pamoja na matokeo ya mitihani ya ndani ya mwezi Januari na februari .
Katika tathimini hiyo Afisa Elimu amewapongeza walimu, walimu wakuu, Waratibu Elimu kata pamoja na wadhibiti ubora kwa kufanya kazi kwa weledi na juhudi kubwa kwani hali ya taaluma inapanda .
Aidha, Mwalimu Urassa, amewataka walimu hao Viongozi kwenda kutoa mrejesho kwa walimu wengine kwa lengo la kufanyia kazi mapungufu .
Na amewataka walimu na Waratibu Elimu kata kuhakikisha wanafunzi hawawekewi vipandikizi .
#tukovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.