Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa amewataka wananchi wa Nachingwea kutumia uwepo wa utolewaji wa huduma za Madaktari bingwa katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea kama fursa. Ameyasema hayo alipokua katika uzinduzi wa utolewaji huduma za Madaktari bingwa katika hospitali ya Nachingwea.
Mhandisi Chionda amemshukuru na kupongeza jitihada za Mheshimiwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma za Afya hususani katika Wilaya ya Nachingwea kwa kuleta fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya Afya na huduma zake.
Aidha, Mhandisi Chionda ameipongeza jitihada za dhati zilizofanywa na Halmashauri ya Nachingwea za kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais kwa kujenga Wodi grade 1 katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea kwani wodi hiyo itawapa watu fursa ya kupata huduma na kuongeza pato kwa Halmashauri hiyo. Wodi hiyo imegharimu Shilingi millioni 175 za mapato ya ndani.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.