Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Chionda Kawawa, ameongoza kikao cha kwanza cha maandalizi ya Tamasha la One Stop Center, Oktoba 11, 2025, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nachingwea,

Katika kikao hicho, wajumbe wamejadili mbinu bora za kuboresha tamasha hilo ili liwe na ubora na mafanikio makubwa zaidi kuliko mwaka uliopita, Pia wamejadili bajeti ya maandalizi ya tamasha zima kwa pamoja,
Mhandisi Kawawa, amewahimiza wananchi kutumia ipasavyo fursa hiyo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, sambamba na kujipatia kipato kupitia biashara, Amebainisha kuwa wajasiriamali wakubwa na wadogo watapata nafasi ya kushiriki kwa kuuza na kutangaza bidhaa zao,
Aidha, kwa makubaliano ya pamoja ya wajumbe wa kikao, tarehe ya tamasha imebadilishwa kutoka Oktoba 1–3, 2025, na sasa rasmi tamasha litafanyika kuanzia Oktoba 4–6, 2025,
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii Bi Stella Kategile, amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni kuja kushiriki na kunufaika kwa pamoja na huduma zitakazotolewa, lengo ikiwa ni kuwafikia wananchi wote wa mjini na vijijini,
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.