Shule ya Sekondari misufini iliyopo kata ya Mpiruka imepokea fedha kiasi cha Milioni 37 .8 kwaajili ya ujenzi wa choo na umaliziaji wa maabara ya shule hiyo
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea ametembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua hatua za ujenzi na kuona uhalisia wa kazi na thamani ya fedha .
DED Chionda amemtaka Mkuu wa shule hiyo kuhakikisha ujenzi wa choo na maabara unakamilika kabla ya Aprili 30, 2024 sambamba na matumizi sahihi ya fedha .
Aidha, ametumia fursa hiyo ya kuzungumza na waalimu kufahamu changamoto zao ambapo walieleza moja ya changamoto kubwa ni madai ya fedha za likizo na kupanda madaraja . Majibu ya maswali hayo yalitolewa na kaimu Afisa Elimu Sekondari Ndugu Humphrey kalisa kuwa bajeti ya elimu sekondari imeombwa kuongezeka kwa mwaka mpya wa fedha ambapo itakuwa na uwezo wa kulipa madeni na likizo kwa wakati .
Eng . Chionda licha ya kuwapongeza walimu hao amewasihii kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kutumia lugha ya kiingereza ipasavyo kama lugha rasmi katika eneo la shule kwa kufundishia na mawasiliano .
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.