Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Mohamed Hassan Moyo ameewaagiza watendaji wa kata wa Halmashauri ya Nachingwea kuwashirikiana na idara ya Elimu Msingi na Sekondari katika kutafuta taarifa za lishe na takwimu za watoto wanaopata chakula Shuleni katika maeneo yao. Kwa kufanya hivyo watendaji wataweza kupata taarifa sahihi za lishe zitakazowawezesha wataalamu wa afya kuzifanyia kazi kwa ufasaha na kusaidia watanzania. Hayo ameyasema leo Julai 18, 2023 alipokua katika kikao cha Lishe cha robo ya mwisho (April - June) ya mwaka wa fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Nachingwea.
Aidha, Mhe. Moyo amewasisitiza watendaji wa kata kuendelea kusimamia ratiba ya maadhimisho ya siku ya afya na lishe vijijini ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika katika maadhimisho hayo. Pia Mkuu wa Wilaya amewataka wataalam wa afya na lishe kuwafuata wananchi katika maeneo yao ya makazi na kuwapa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa lishe kwani ni idadi ndogo sana ya wananchi wenye ufahamu wa umuhimu wa lishe.
Kwa upande wake Bi Juliet Mkania ambae ni Mratibu wa Afya ngazi ya jamii amesema watoa huda kwa ngazi ya jamii wapewe fomu mapema ili waweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
#tupovizuri
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.