MKuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wazazi na walezi kukemea na kupinga mapenzi ya jinsia moja( ushoga na usagaji) ili kujenga kizazi bora kwa faida ya Taifa.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi katika kanisa la kambi la waebenia lililopo Kijiji cha matangini kata ya Nangowe, Moyo alisema kuwa waamuni,wachungaji na maaskofu wanatakiwa kupinga vilivyo vitendo vya ushoga kwenye jamii ili kuwa na watoto walio bora.
"Baba mchungaji,baba askofu naombeni pingeni kwa nguvu zote vitendo vya ushoga na usagaji vinaharibu watoto wetu ulisikia wapi Mungu aliruhusu mapenzi ya jinsia moja,nawaombeni kwa dhati mkemee kwa vitendo Jambo hilo"alisema Moyo
Amewahasa Wazazi na Walezi kulea Watoto wao kwa kuzingatia maadili mema ya kitanzania pamoja na kuwa makini na maudhui ya Watoto (Katuni) katika simu na televisheni ili kuwaepusha na kujifunza mambo yasiofaa na kutambua marafiki wa watoto wao na kuwapa miongozo sahihi wakati wote.
Pia amewataka Walimu wa Shule za Msingi, Sekondari na hata Vyuoni kukemea kwa nguvu uharibifu wa maadili ya kitanzania katika maeneo ya kutolea elimu.
Aidha Moyo alimazia kwa kusema kuwa atawachangia kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo la kambi la waebenia lililopo Kijiji cha matangini kata ya Nangowe wilaya ya Nachingwea.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.