Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amekutana na Maafisa mifugo, tarafa pamoja na Maafsa kilimo Julai 1, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mhe Moyo amewata Maafsa hao kuorodhesha faida na mafanikio katika kipindi kilchopita na kipindi cha sasa pia amewaagiza kusimamia kikamilifu masuala ya wafugaji ili kudhibiti wasiingie kwa njia za panya, pia amewataka kua waalimu katika matumizi ya uzio wa pilipili na mizinga ya nyuki kwa lengo la kuzuia uharibifu wa mazao dhidi ya wanyama wakali Tembo na wahakikishe chakula hakichabganywi na madawa katika maghala ya mazao ya kila eneo ni lazima kuwe na shamba darasa.
Aidha, Bwana Raphaeli Ajetu ambae ni Mmuu wa Idara ya kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmshauri ya Nachingwea amewataka Maafsa hao kuwa na matumizi sahihi ya pikipiki walizopewa na ufuatiliaji wa taarifa sahihi za wakulima na usimamiaji mashubuti wa uingiaji wa wafugaji kiholela pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii juu ya udhibiti wa wanyama poli ambao wanaharibu mazao mashambani
Kwa upande wake Glory Ndekirwa ambae ni Afsa Wanyamapori ameeleza kuwa ameiomba wizara husika kushughulikia suala la kifuta jasho na machozi kwa wahanga wa tukio hilo liwe la haraka sambamba na kuwaomba Maafsa hao utoaji wa taarifa sahihi za wahanga hao lengo ikiwa ni kufuatilia kwa urahisi Malipo yao ya kifuta jasho hcho.
#tupovizuri
@wizara_ya_kilimo
@bashehussein
@moddymoyo5
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.