Nachingwea, 24 Septemba 2024 – Watendaji wa vijiji katika wilaya ya Nachingwea wamefanya kongamano katika ukumbi wa TTC, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwda Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Moyo alisisitiza umuhimu wa kazi inayofanywa na watendaji hao katika kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao, pia amekiri kuwa wana mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya jamii, huku akiwapongeza kwa juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya.
“Napenda kuwapongeza kwa kazi yenu nzuri, Miradi mnayosimamia inaboresha maisha ya wananchi wetu, pia amewataka kuzingatia miongozo na taratibu za utumishi wa umma ili waweze kufanya kazi kwa weledi,” alisema Mheshimiwa Moyo.
Kongamano hilo pia lililenga kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili watendaji wa vijiji, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa rasilimali na mahitaji ya mafunzo zaidi, watendaji walipata fursa ya kubadilishana mawazo ya kufanikisha mikakati ya kutatua matatizo yanayowakabili.
Mheshimiwa Moyo aliwataka watendaji hao kuimarisha ushirikiano na jamii, na kuhimiza uwazi katika maamuzi yao ili kujenga uaminifu miongoni mwa wananchi, Kongamano hili ni ishara ya dhamira ya watendaji wa vijiji katika wilaya ya Nachingwea ya kuimarisha utendaji wao na kuleta mabadiliko chanya.
Copyright ©2018 Nachingwea District Council. All rights reserved.